Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe Said Thabit Mwambungu amesema kuwa Serikali inathamini mchango mkubwa unaotolewa na waandishi wa habari katika ujumbe wa serikali kwa wananchi ili kusukuma gurudumu la maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Said Mwambungu akiongea na waandishi wa habari Ofisi kwake
Mhe. Mwambungu amesema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wa Manispaa ya Songea Ofisini kwake hivi karibuni
Aidha, Mkuu wa Mkoa huyo amewataka waandishi hao wa habari kuendelea kuhabarisha Umma wakizingatia maadili ya habari kwani kwa kukiuka maadili wanaweza kuipotosha jamii na kusababisha hatari katika jamii.
Kwa upande wake Katibu wa Ruvuma Press Club Bw. Andrew Chatwanga amempongeza Mkuu wa Mkoa kwa uamuzi wake wa kuongea na wanahabari hao ikiwa ni siku chache tu baada ya kuripoti mkoani kuanza kazi ya kuongoza shughuli za Serikali mkoani hapo.
Bw. Chatwanga alitumia fursa hiyo kumwomba Mkuu wa Mkoa kuchukua hatua za kipekee ili kuifanya Manispaa ya Songea inaboreka kwa usafi wa mazingira kama alivyofanya kwa Manispaa ya Morogoro. Kwa sasa Manispaa ya Songea usafi wa mazingira hauridhishi.
Habari hii ni kwa hisani ya Revocatus A. Kasimba, Afisa Habari, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa
No comments:
Post a Comment