Monday, April 22, 2013

Flag this message UJIO WA WADAU WA MAENDELEO MKOANI MWANZA


Na:  Atley  Kuni - Afisa Habari Mkoa wa Mwanza.

Leo kubwa katika Mkoa wa Mwanza tumepokea Ugeni wa Wadau wa mashirika ya Maendeleo kutoka (DPG), Ambalo linajumuisha balozi zote zilizopo hapa nchini, Zikiwapo Jumuiya ya Ulaya,Wakuu wa Mashirika ya Ufadhili, wa Maendeleo kama NDP, WB, AFDB, JICA UNICEF.

Ujumbe huu umefika Mkoani hapa na Kuonana na Vingozi wa Mkoa wa Mwanza, akiwapo Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na watendaji wengine wa Mkoa na Halmashauri za Wilaya na Wataalam wengine wa taasisi za umma zilizopo katika  Mkoa huu.

 Katika ziara yao hiyo, wamepata kusikia Speach kuhusu Masuala Mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa huu. Lengo la Ziara Hiyo ilikuwa Kutembelea na kuona jinsi Miradi mbalimbali ya maendeleo inavyo tekelezwa, hivyo wametembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo katika Mkoa huu ikiwapo,  Mradi wa barabara za Mawe, unao tekelezwa katika Mkoa huu hususan katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

 Hata hivyo kwa mujibu wa ratiba yao siku tarehe 23/4/2013, watafanya ziara katika Mkoa wa Geita.

Kuhusu mambo mengine Mwanza ni salama, Mvua zipo za wastani, na jua linawaka kwa Mbali.






Flag this message UJIO WA WADAU WA MAENDELEO MKOANI MWANZA


Na:  Atley  Kuni - Afisa Habari Mkoa wa Mwanza.

Leo kubwa katika Mkoa wa Mwanza tumepokea Ugeni wa Wadau wa mashirika ya Maendeleo kutoka (DPG), Ambalo linajumuisha balozi zote zilizopo hapa nchini, Zikiwapo Jumuiya ya Ulaya,Wakuu wa Mashirika ya Ufadhili, wa Maendeleo kama NDP, WB, AFDB, JICA UNICEF.

Ujumbe huu umefika Mkoani hapa na Kuonana na Vingozi wa Mkoa wa Mwanza, akiwapo Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na watendaji wengine wa Mkoa na Halmashauri za Wilaya na Wataalam wengine wa taasisi za umma zilizopo katika  Mkoa huu.

 Katika ziara yao hiyo, wamepata kusikia Speach kuhusu Masuala Mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa huu. Lengo la Ziara Hiyo ilikuwa Kutembelea na kuona jinsi Miradi mbalimbali ya maendeleo inavyo tekelezwa, hivyo wametembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo katika Mkoa huu ikiwapo,  Mradi wa barabara za Mawe, unao tekelezwa katika Mkoa huu hususan katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

 Hata hivyo kwa mujibu wa ratiba yao siku tarehe 23/4/2013, watafanya ziara katika Mkoa wa Geita.

Kuhusu mambo mengine Mwanza ni salama, Mvua zipo za wastani, na jua linawaka kwa Mbali.






UJIO WA WADAU WA MAENDELEO MKOANI MWANZA


Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Dorothy Mwanyika akitoa neno la utambukisho kwa ugeni wa Wadau wa mashirika ya Maendeleo kutoka (DPG)


Mtaalamu kutoka Wizara ya Fedha akifafanua jambo

Barabara ya Mawe ya Igogo kama inavyoonekana Jijini Mwanza

Sunday, April 21, 2013

WANAFUNZI WAPATA AJALI YA GARI MWANZA

Na. Afisa Habari Mkoa wa Mwanza 

Jumla ya wanafunzi wapatao ishini na saba wamejeruhiwa vibaya kufuatia ajali mbaya iliyo lihusisha garia aina ya Roli lililokuwa likisafiri kutoka Kasororo kwenda Misasi kwenye shughuli za Umiseta.
 
Kwa mujibu wa taarifa fupi iliyotolewa na Afisa Michezo wa Sekretarieti ya Mkoa wa Mwanza, nikuwa gari hilo lilikuwa likiwasafirisha wanafunzi kwenda kwenye Michezo ajali imetokea katika Tarafa ya Mbarika Wilaya ya Misungwi Mkoani hapa.
Majeruhi 12 wamelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Missungwi na kumi na watano(15), walikimbizwa katika hospitali ya Rufaa Bugando kwa Matibabu zaidi.
 
Taarifa hiyo imesema pia kuwa hali ya Majeruhi mmoja sio nzuri sana kwani sehemu kubwa ya kichwa ndio iliyojeruhiwa vibaya, huku mwalimu mmoja ambaye hakuweza kufahamika mara moja akiwa amechanwa na kitu kinacho zaniwa kuwa ni chuma sehemu ya kifua.
Hata hivyo Ninaendelea kufatilia juu ya tukio hili na habari kamili juu ya Majina ya Majeruhi hao nitawatumia kupitia mtandao wetu wa Mawasiliano.

Monday, April 15, 2013

AGA KHAN YATOA HUDUMA KWA KAMBI


Kituo cha Afya cha Aga Khan Iringa kwa kushirikiana na Serikali kimetoa huduma za afya ya mama mjamzito na mtoto katika wilaya ya Mufindi na kufanikiwa kuwahudumia wananchi wengi kwa wakati mmoja.

Katika mahojiano na Mratibu wa Mradi wa Tuunganishe Mikono Pamoja nchini, Narmin Adatia katika kituo cha afya cha Ihongole amesema “lengo la kuweka kambi katika kituo cha afya cha Ihongole ni kuhakikisha tunawafikia wananchi wengi zaidi kwa wakati mmoja na kuhakikisha wananchi wananufaika na huduma ya afya ya mama mjamzito na mtoto”. Amesema tumeamua kuweka mguvu zaidi kwa wanawake wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kwa sababu kundi hilo linahitaji huduma bora na salama zinazopatikana kwa urahisi na ukaribu katika maeneo yao. Amesema kufanya hivyo kunasaidia kufikia malengo ya Milenia katika kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Akiongelea ushirikiano baina ya Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na sekta binafsi, Narmin amesifu ushirikiano huo unaogusa ngazi zote za Serikali. Ameishukuru Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kupitia Ofisi ya Mganga Mkuu wa wilaya kwa kuwachagulia eneo kwa ajili ya kuweka kambi wilayani hapo ili kuwafikia wananchi wengi zaidi wilayani Mufindi katika kituo cha Afya cha Ihongole.

Nae Diwani wa Kata ya Boma, Raphael Makomba amesema kuwa hilo ni jambo jema lililolenga kuwahudumia wananchi wengi zaidi kwa wakati mmoja. Amepongeza jitihada za kituo cha afya cha Aga Khan kupitia mradi wake wa Tuunganishe Mikono Pamoja kwa kushirikiana na Serikali ya Wilaya ya Mufindi kuamua kupeleka huduma hiyo katika Kata ya Boma. Ametumia fursa hiyo kuomba huduma hiyo iwe endelevu ili kuendelea kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa wakati mmoja.

Morris Mwingila, mama mjamzito aliyekwenda katika kambi hiyo
kwa ajili ya kupata huduma ya afya amesifia huduma hiyo na kusema kuwa watoa huduma walikuwa wamejipanga kikamilifu kuwahudumia wananchi kwa haraka na ubora. “Nilitarajia kuwa watu tutakaa muda mrefu katika mistari tukisubiri huduma lakini imekuwa tofauti, watoa huduma wamekuwa wakitoa huduma kwa haraka sana” alisisitiza Morris.

Huduma ya Afya kwa Mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano imetolewa bure na kituo cha Aga Khan Iringa katika kituo cha afya cha Ihongole kwa kushirikiana na Wilaya ya Mufindi ikiwa ni muendelezo wa huduma hizo chini ya mradi wa Tuunganishe Mikono Pamoja. Huduma zilizotolewa ni pamoja na uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi, unasihi, uzazi wa mpango, upimaji wa CD4 na magonjwa mengine mengi.
=30=

Saturday, April 13, 2013

HUDUMA YA KAMBI CHINI YA MRADI WA TUUNGANISHE MIKONO PAMOJA (JHI)

 Wananchi wa Kata ya Boma akiwa wanajiandikisha kabla ya kuanza kupata huduma za afya katika kituo cha Ihongole kwenye Kambi ya kituo cha aga Khan chini ya Mradi wa Tuunganishe Mikono Pamoja (JHI)

Meneja wa Kituo cha afya Aga Khan Veronica James (kushoto) na Mratibu wa mradi wa JHI Narmin Adatia (kulia) wakiweka mikakati ya kuboresha huduma katika kambi 

 Muuguzi akimhudumia mgonjwa katika kituo cha afya Ihongole

Wananchi wakisubiri huduma ya tiba katika kituo cha afya cha Ihongole 

Morris mwingila akipata huduma ya kipimo katika Kituo cha afya cha Ihongole

Thursday, April 11, 2013

TAFRIJA YA KUMUAGA KATIBU TAWALA MKOA WA IRINGA MSTAAFU

 RAS mstaafu Mkoa wa Iringa Gertrude Mpaka (kushoto) akimlisha keki Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Pudenciana Kisaka.

RAS mstaafu Gertrude Mpaka (kushoto) Mkoa wa Iringa, akimlisha keki Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi,Edna Kaduma.

 RAS mstaafu Mkoa wa Iringa Gertrude Mpaka (kushoto) akimlisha keki Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Mohamed Gwalima


RAS Mkoa wa Iringa mstaafu Gertrude Mpaka (kushoto) akimlisha keki Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo.


RAS mstaafu Gertrude Mpaka (kushoto) Mkoa wa Iringa, akimlisha keki Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Joseph Muhumba



RAS mstaafu Gertrude Mpaka (kushoto) Mkoa wa Iringa, akimlisha keki Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Stephen Mhapa

RAS mstaafu Gertrude Mpaka (kulia) Mkoa wa Iringa, akimlisha keki Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi