Friday, September 13, 2013

MWALIKO WA TAMASHA LA 'MTAKUJA' KWA WADAU WA ELIMU NA WASANII




Uongozi wa shule ya Sekondari Mtakuja iliyopo Kunduchi, Dar-es-salaam, unayo furaha kukukaribisha wewe ukiwa kama mdau wa elimu na burudani katika Tamasha la Wanafunzi (2013 School Bash) litakalofanyika shuleni hapo siku ya kesho Jumamosi kuanzia saa mbili asubuhi.

Tamasha hilo linatarajiwa kuhusisha shule zaidi ya 20 na wanafunzi zaidi ya 1000. Kutakuwa na 'activities' mbali mbali za kielimu, kimichezo na kiburudani. Wewe ukiwa kama mdau wa mojawapo wa activities hizo, unakaribishwa. 

Wasanii wa muziki ambao ndio hupendwa zaidi na wanafunzi, nao wamealikwa bila kujali ni msanii mkubwa au mdogo. Uwepo wako utathaminiwa sana na utafurahiwa sana na wanafunzi. Utapewa nafasi bila hiyana kujihusisha nao moja kwa moja kwa kuwaburudisha au kuzungumza na kujadiliana nao kwa njia yeyote ile. Kumbuka pia lengo la Tamsha hili ni kukuza mkakati wa taifa unaoendelea hivi sasa hasa kwenye sekta ya elimu wa 'Big Results Now'.

Tumia fursa hii kukutana na mashabiki wako wanafunzi na wadau wengine mbali mbali, katika kuendelea kujijengea jina jema kwa vijana hawa wadogo wanaokua.

Imetolewa na:

Misonji Charles (0714642442)
Muandaaji wa Tamasha.

No comments:

Post a Comment