JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA
SERIKALI ZA MITAA
|
|
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,
S. L. P. 320,
Shinyanga
10 Februari, 2014
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
TSHS.BILIONI 16
ZATUMIKA KUTEKELEZA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI JULAI – DESEMBA 2013
Mkoa
wa Shinyanga umetumia jumla ya Shilingi 16,097,445,854
kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kipindi cha Mwezi Julai hadi Desemba Mwaka 2013.
Fedha
hizo zimetumika katika sekta mbalimbali kama ilivyoainishwa katika maelekezo ya
Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya uchaguzi mkuu na malengo yaliyopangwa
kutekelezwa kwa kipindi hicho.
Utekelezaji
wa Ilani umezingatia malengo ya Mpango wa Matokeo Makubwa sasa na malengo ya
maendeleo ya milenia hadi ifikapo 2015.
Katika
kipindi cha nusu ya mwaka 2013/2014, mafanikio makubwa yamepatikana katika
sekta za Elimu,Afya,Maji,Kilimo,Miundombinu, Mapato ya Ndani ,Mifugo n.k. kama
ifuatavyo:-
Mapato ya ndani
Hadi
kufikia Desemba 2013 mkoa umekusanya mapato ya ndani kiasi cha Sh. 5,983,590,960 sawa na asilimia 47.3 ya Lengo kwani Mkoa
umejiwekea Lengo la kukusanya kiasi cha Sh.11,356,021,186
kwa mwaka wa Fedha 2013/14.
Elimu
Kwa
kipindi cha miezi sita,upande wa Elimu ya msingi,serikali imefanikiwa kuongeza
madawati 1692, kusambaza vitabu 157,051 katika shule zote, kujenga nyumba za
walimu 31 kujenga matundu ya vyoo 136 na madarasa 38 kwa Tshs 2,991,101,190 sawa na ongezeko la
asilimia 40 ya mwaka jana 2012/2013.
Aidha, madawati 459 kwa ajili ya madarasa
ya awali yametengenezwa na ununuzi bado unaendelea,vilevile jumla ya watoto
3070 wenye ulemavu walimbuliwa na kuandikishwa katika Elimu ya Msingi.
Katika
Elimu ya sekondari,Mkoa umetumia jumla ya Tshs. 1,348,013,030 kusambaza madawati, kujenga vyumba14 vya maabara na
vifaa vya maabara hizo, kujenga maktaba na kununua vitabu 2975, kujenga nyumba
za walimu 4, kujenga madarasa 17 na vyoo matundu 23.
Afya
Katika
sekta ya Afya serikali imetumia kiasi cha Tsh.3,464,084,797 katika kuajiri watumishi 145 wa kada
mbalimbali,kukarabati vituo vya Afya15,nyumba 11 za watumishi wa sekta ya Afya,
ujenzi wa zahanati 40 unaendelea,ununuzi wa vifaa tiba,ujenzi wa hospitali ya
wilaya unaoendelea, ununuzi wa gari moja la wagonjwa,usafirishaji wa wagonjwa
520 kwenda hospitali za rufaa, ujenzi wa jengo la OPD na kufanya matengenezo ya magari yanayotumika
kwa ajili ya ufuatiliaji na usimamizi wa huduma za Afya.
Maji
Tshs.
6,064,397,831 zimetumika katika kuboresha sekta ya maji kwa shughuli
zifuatazo:- kujenga miradi ya maji
ya visima virefu 17 ikiwa ni pamoja na kutandika mabomba na kufunga pampu za
mikono kwenye visima virefu, mafunzo mbalimbali yamefanyika na vikundi vya maji
19 vilivyoundwa na kaya 115 kuhusu uvunaji wa maji ya mvua.
Aidha vituo 42 vya
kuchotea maji vimejengwa, mabirika 67 ya kunyweshea ng’ombe yamejengwa, visima
vifupi 15 vimechimbwa sambamba na uchambaji wa mitaro ya kulaza mabomba.
Serikali ipo katika mchakato wa
kupeleka huduma ya maji katika wilaya ya Kishapu kutoka
bomba kuu la maji ya Ziwa Viktoria.Tayari michoro ya kupeleka maji imekamilika
na kazi inayoendelea sasa ni kupata mkopo kwenye taasisi za fedha na pia
kushirikiana na mgodi wa Almasi wa Mwadui.
Kilimo
Kiasi
cha Tshs.1,557,687,000 zimetumika
kufanikisha mapinduzi ya kilimo ikilinganishwa na tshs.907,664,635
zilizotumika mwaka 2012/2013 sawa na ongezeko la asilimia 58 ikilinganishwa na
kipindi cha Januari hadi Juni 2013.Shughuli zilizofanyika katika kipindi hiki
ni pamoja na ufuatiliaji wa mashamba darasa ya wakulima, ujenzi wa vituo vya
rasilimali za kilimo, kuanzisha mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora, kuongeza
upatikanaji wa pembejeo, kununua vikatuzi nguvu yaani Power Tillers” 6, jumla
ya vocha 8441 zimsambazwa, mbegu bora za mtama aina ya Macia zimesambazwa tani
12.7,kata 20 zimehamasishwa kulima mazao yanayostamili ukame,vyama vitatu vya
SACCOS vimepewa mafunzo na zana za kilimo na ujenzi wa miundombinu ya
umwagiliaji.
Ufugaji
Katika sekta ya ufugaji
zimetumika shilingi 148,530,310 kutoa mafunzo ya ugani kwa wafugaji
3431,kujenga malambo matatu,na jumla ya mifugo 33,686 imepatiwa chanjo. Aidha, vikundi 38 vya wafugaji
vimeundwa kufikia Desemba 2013.
Wanyamapori na
Misitu
Tsh.4,656,000 zimetumika kuunda vikundi 7 vya
mtandao wa ushirika wa ufugaji wa nyuki,mikutano ya hamasa juu ya kufuga kwa
kutumia mizinga ya nyuki ya kisasa imefanyika katika kata 24, kuandaa na kutoa
mizinga ya kisasa 1641 kwa ajili ya kujifunzia, kuendeleza msukumo katika
ufugaji wa nyuki na kutoa Elimu kwa wafugaji nyuki.
Mkoa
unaendelea na juhudi za kulinda na kuhifadhi mazingira ikiwa ni pamoja na
kutunza vyanzo vya maji. Jumla ya miti 126,000 imeoteshwa na kupandwa na watu
binafsi na shule za msingi.
Miundombinu
Kwa
kipindi cha miezi sita,serikali imetumia shilingi 1,126,973,000 kufanya shughuli za kutoa hatimiliki za kimila na
ugawaji wa ardhi.Matengenezo ya kawaida ya barabara katika sehemu korofi jumla
ya km 539.52, usanifu wa ujenzi wa kiwango cha lamo wa km 15,uchimbaji wa
mitaro ya maji ya mvua yenye ukubwa wa ujazo wa(cubic meter) 6100 matengenezo
makalavati jumla ya mistari 21.
Aidha,
uwanja wa ndege wa Ibadakuli upo kwenye mchakato wa kuboreshwa kwa kiwango cha
lami kwenye njia ya ndege,kujenga ghorofa moja la abiria na maegesho ya magari
madogo. Ujenzi huo utagharimu shilingi Bilioni 17 na tayari zabuni ya kumpata
Mhandisi mshauri imetangazwa.
Utawala Bora
Ili
kudumisha utawala bora wenye kufuata misingi ya haki na usawa, kiasi cha
shilingi 197,045,196 zimetumika
kuendesha vikao vya kamati za maendeleo ya kata, mabaraza ya wafanyakazi na
mabaraza ya madiwani.
Ulinzi na Usalama
Hali
ya ulinzi na usalama katika mkoa ni ya kurdhisha tofauti na kipindi cha nyuma
kwani matukio makubwa ya uhalifu yamepungua,kwa kipindi cha Julai-Desemba,2013
mauaji ya Albino na yale yanayohusishwa na ushirikina yamepungua kwa asilimia
99 ikilinganishwa na asilimia 95 ya kipindi kilichopita.
Mkoa
umewaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri kutenga fedha kwenye bajeti ya 2014/14
kwa ajili ya mgambo na ujenzi wa vituo vya polisi na Mahakama katika maeneo yao
ya utawala ili kuimarisha haki, ulinzi na usalama.
Kuendeleza
makundi maalum ya Wanawake,Watoto,Vijana na Walemavu
Katika
kudumisha shughuli na ustawi wa makundi maalumu, shilingi 102,738,000
zimetumika kuimarisha mifuko ya uwezeshaji wa wanawake na kuhamasisha vyama vya
kuweka na kukopa(SACCOS na VICOBA),vikundi 12 vya wanawake
vimeelimishwa,vikundi 75 vimesajiliwa na kupewa mafunzo ya kuimarisha mifuko ya
mikopo,vikundi 20 vya wanawake wajasiriamali vimewezeshwa kwa mikopo na
kurejesha mikopo hiyo.
Vilevile, Mkoa umesimamia Halmashauri kutoa michango ya
asilimia 5 kwenye mfuko wa maendeleo ya wanawake.
Aidha,
mkoa umefanya juhudi kubwa katika kuhakikisha kwamba haki za watoto
zinasimamiwa ipasavyo kwa kutoa Elimu katika vijiji 32 kwa kushirikiana na mashirika
ya Save the Children, AMREF na UMATI / JOICEF.
Vikundi
12 vya vijana wajasiriamali na ushirika wa kuweka na kukopa yaani SACCOS na
VIKOBA vimeanzishwa na usimamizi wa matumizi ya fedha za maendeleo ya vijana
umeimarishwa ili kuwanufaisha vijana wengi zaidi,na kuhakikisha asilimia 5 ya
mfuko wa vijana inatengwa.
Kwa
upande wa walemavu jumla ya shilingi 4,120,000 zimetumika kuwaendeleza pamoja
na kuwaandikisha watoto wenye ulemavu na wenye uhitaji maalum. Watoto 3,070
wenye mahitaji maalum wametambuliwa na kuandikishwa darasa la kwanza.
Elimu
ya ujasiriamali imetolewa kwenye vikundi 6 vya watu wenye ulemavu,pia walemavu
wamewezeshwa katika maadhimisho ya sherehe zao za siku ya fimbo nyeupe, siku ya
walemavu duniani na siku ya Albino.
Viwanda
Mkoa
unaendelea na juhudi za kuendeleza viwanda pamoja na kutangaza fursa za
uwekezaji nje na ndani ya nchi yetu.Hadi Desemba 2013 hali halisi ya viwanda
ilikuwa kama ifuatavyo:-
§
Kiwanda
cha ngozi cha Xinghua Investment Co.Ltd
kilikuwa kimekamilika hivyo mwekezaji alikuwa anatarajia kujaribu mitambo mwezi
Januari 2014, kabla ya kuanza uzalishaji na mwezi huu Februari kimeanza
uzalishaji.
§
Kiwanda
cha nyama cha Xinghua Investment
kinatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka huu 2014.
§
Mwekezaji
Dahong Cotton Product Limited amekamilisha kiwanda cha
kuchambua nyuzi za pamba klichopo Nhelegani.
§
Kiwanda
cha kukamua mafuta ya kupikia ya pamba cha Jielong
Holding (T)Ltd kilichopo Nhelegani pia kimekamilika.
Serikali
ya mkoa wa Shinyanga inazidi kuwahimiza wananchi kuendelea kushirikiana na
viongozi wao kuanzia ngazi za vijiji na mitaa,kata,tarafa na wilaya katika
kuibua na kutatua changamoto zinazowakabili kwenye maeneo yao, na changamoto
zinazohitaji ushauri wa ngazi ya mkoa zifike na zitaendelea kushugulikiwa.
Imetolewa
na
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga