Wednesday, January 31, 2018

MASENZA AIHAKIKISHIA KAMATI YA BUNGE USALAMA IRINGA



Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa- Iringa
Kamati ya Bunge ya utawala na serikali za mitaa imehakikishiwa kufanya kazi kwa amani na usalama mkoani Iringa kutokana na vyombo vya usalama kuwa macho muda wote.

Uhakika huo ulitolewa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akiongea na kamati ya Bunge ya utawala na serikali za mitaa katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa Mkoa, kamati hiyo ilipofanya ziara mkoani hapa.
 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza (kusho), kulia ni Mwanne Mchemba, Makamu Mwenyekiti Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa
Masenza ambaye pia ni mkuu wa Mkoa wa Iringa alisema kuwa Mkoa wa Iringa upo shwari. Hali ya usalama ni nzuri kuiwezesha kamati hiyo kufanya ziara ya kikazi katika hali ya usalama na utulivu. Aidha, aliongeza kuwa wananchi mkoani Iringa wanajitambua katika kutekeleza majukumu yao. 

Wananchi mkoani Iringa hasa wakulima katika msimu huu wa kilimo wanajitambua na hawashurutishwi kutekeleza majukumu yao ya kilimo” alisema Masenza.

Wakati huohuo, makamu mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya utawala na serikali za mitaa, Mwanne Mchemba alisema kuwa dhumuni la ziara ya kamati yake ni kukagua miradi ya maendeleo wilayani Kilolo kwa fedha zilizotolewa na serikali mwaka 2016/2017. 

Tunajua kuwa mkuu wa Mkoa ni jembe katika usimamizi wa uhamasishajai wa maendeleo. Hivyo, kamati inataka kujiridhisha na matumizi ya fedha za serikalai hasa thamani ya fedha kabla ya serikali kuidhinisha fedha nyingine kwa Wilaya ya Kilolo” alisema Mchemba.    
=30=

RC MASENZA ASHAURI MATUMIZI YA TEHAMA MAHAKAMA KUU IRINGA



Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza ameishauri Mahakama kuu kanda ya Iringa kuongeza kasi ya matumizi ya Tehama katika utoaji wa haki kwa wananchi.

Kauli hiyo aliitoa katika salamu zake kwenye uzinduzi wa wiki ya sheria nchini uliofanyika katika uwanja wa Mahakama kuu Iringa jana.
 

Masenza alisema kuwa faida za Tehama katika Mahakama ni kurahisisha utoaji haki kwa wakati kwa wananchi. Aliongeza kuwa Tehama inasaidia kutunza kumbukumbu muhimu za mwenendo wa kesi na hatimae utolewaji wa haki. 

Tehama inaimarisha mawasiliano miongoni mwa wadau. Ni rahisi kuwapa taarifa wadau huko waliko wakahudhuria Mahakamani kwa wakati pale wanapohitajika bila taarifa kupotea. Tehama huimarisha maadili ya utoaji wa haki kwa wananchi, vifaa kama CCTV camera na vifaa vingine vya aina hiyo ni muhimu katika kuimarisha maadili ya haki” alisisitiza Masenza.

Katika hotuba ya Jaji mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Iringa, mheshimiwa Mary Shangali alisema kuwa wiki ya sheria nchini imelenga Mahakama kujipambanua kwa wananchi na kueleza majukumu ya Mahakama na kutoa elimu kwa wananchi kuwa mahkama kuu ya Tanzania ipo kwa ajili ya wananchi na haki zao.

Mheshimiwa Shangali aliongeza kuwa wiki hiyo inalenga kupima utendaji kazi wa Mahakama. Alisema katika maadhimisho hayo, vituo vya kutolea elimu na kupokelea maoni ya wananchi vimeandaliwa katika shule ya sekondari ya wasichana Iringa, shule ya sekondari ya Miyomboni na chuo kikuu cha Iringa.
=30=    
  

Sunday, January 28, 2018

MATOKEO YA MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU KWA TAASISI MKAONI IRINGA




NA
TIMU
1
RAS IRINGA  1-0  IRUWASA
2
MAGEREZA  0-0  TANROADS
3
MKWAWA 4- 2 KLERUU
4
KIUMAKI 5-1 SIDO
5
DIRA  3-I  IRUWASA
6
AIRPORT  3-0  POSTA
7
TRA  1-1  MAGEREZA

Sunday, January 21, 2018

MATUKIO KATIKA PICHA UFUNGUZI MICHEZO YA TAASISI MKOA WA IRINGA

TIMU YA RAS IRINGA WAPOTEANA UWANJANI BAADA YA KICHAPO CHA 5-0 TOKA TANROADS



Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  
Timu ya mpira wa miguu ya RAS Iringa imechapwa magoli 5-0 na  wakala wa Barabara (TANROADS) katika mechi ya ufunguzi iliyoshuhudiwa na mamia wa wakazi wa Manispaa ya Iringa wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela.

Mechi hiyo iliyochezwa katika dimba la chuo cha Ualimu Kleruu kilichopo manispaa ya Iringa ilianza kwa kasi ndogo huku kila timu ikosoma mchezo wa mwezake. Hadi kipinci cha kwanza kinaisha timu ya RAS IRINGA ilikuwa nyuma kwa goli Moja. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kidogo. 
 
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akisalimiana na Peter Nyakigera
Jitihada za RAS IRINGA kurudisha goli zilionekana wazi kabla ya juhudi hizo kufifishwa baada ya golikipa wao namba moja Mashaka Mwanage kuumia mkono wa kuume na kushindwa kuendelea na mchezo. Pigo hilo kwa RAS IRINGA lilifungulia mvua ya magoli hadi kufikia magoli matano.

Tangu awali TANROADS walionekana kukamia mechi hiyo huku wakiwa na kikundi cha washangiliaji mahili. Muda wote wa mchezo meneja wa TANROADS Mhandisi Daniel Kindole alikuwa akifuatilia kwa makini mechi hiyo.

Baada ya kipeng cha mwisho watumishi wa RAS walionekana kuondoka mmoja mmoja kwa njia yake jambo lililotafsiriwa na wachambuzi wa masuala ya soka kuwa ni kuvurugwa na kichapo hicho.
=30=

WATUMISHI WANAOSHIRIKI MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU MKOANI IRINGA WATAKIWA KUCHEZA KWA NIDHAMU



Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Watumishi wa taasisi mbalimbali mkoani Iringa wametakiwa kucheza kwa nidhamu na kuepuka ugomvi katika mashindano ya mpira wa miguu yanayoendelea mkoani Iringa.

Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza katika hotuba yake ya ufunguzi wa mchezo wa mpira wa miguu kwa taasisi za mkoa wa Iringa iliyosomwa kwa niaba yake na mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela katika uwanja wa chuo cha ualimu Kleruu kilichopo Manispaa ya Iringa jana.
 
Mkuu wa Wilaya y Iringa, Richard Kasesela
Masenza aliwataka wachezaji hao kucheza kwa nidhamu na kuepuka kuchochea ugovi. Alisema kuwa mchezo wa mpira wa miguu ni burudani na unajenga urafiki hivyo, mashindano hayo yatumike kutoa burudani na kujenga urafiki miongoni mwa wanamichezo hao. 

Aliongeza kuwa mashindano hayo yatumike kujenga uzalendo kwa watumishi wa umma na watumishi wa taasisi zisizo za kiserikali mkoani Iringa. Aidha, aliwataka wanamichezo hao kutengeneza mtandao utakaowaunganisha kama wanamichezo na watumishi wa taasisi mbalimbali.

Katika salamu za afisa michezo Mkoa wa Iringa, Kenneth Komba kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, alisema kuwa michezo hiyo ni wazo la mkuu wa Mkoa wa Iringa kutaka kuwaunganisha watumishi wa taasisi za Mkoa wa Iringa kupitia mchezo wa mpira wa miguu. Alisema kuwa hadi kufikia jana jumla ya taasisi 21 zilikuwa zimejitokeza kushiriki mashindano hayo.

Wakati huohuo, mechi ya ufunguzi, timu ya Timu ya RAS Iringa ilikubali kichapo cha magoli 5 bila kutoka TANROADS.

Mashindano ya mpira wa miguu kwa taasisi za Mkoa wa Iringa ni mashindanao ya kwanza ya aina yake kufanyika mkoani hapa yakikabiliwa na changamoto ya udhanimi.
=30=