Na.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
USAID Tulonge Afya
wapongezwa kwa kuchagua kutumia mbinu za mabadiliko ya tabia kwa wanajamii
(Social Behavior Change Communication approach) katika kufanikisha malengo ya
mradi huo.
Pongezi hizo
zilitolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu alipokuwa akifungua
kikao cha kuutambulisha mradi wa USAID Tulonge Afya unaotekelezwa na shirika la
FHI 360 kilichofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Gentle Hills mjini Iringa
jana.
Ayubu alisema kuwa
mradi huo umechagua kutumia mbinu za mabadiliko ya tabia kwa wanajamii (SBCC).
“Nimefurahishwa sana kwa kutambua umuhimu
wa mbinu hii mliyoichagua katika kuleta mabadiliko hasa pale inapotumika kwa
ufasaha” alisema Ayubu.
Aidha, alimtaka meneja mradi wa kanda kusimamia
vizuri mradi huo ili mwisho wa utekelezaji mabadiliko chanya ya tabia za
wananchi yaweze kuonekana.
Katibu
Tawala Mkoa wa Iringa aliutaka mradi wa USAID Tulonge Afya kusaidia kuongeza
kasi katika utekelezaji wa mkakati wa Mkoa wa kupunguza maambukizi mapya ya
virusi vya Ukimwi.
“Natambua pia mkakati
wa Mkoa ni kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI, kuhakikisha
wanaoishi na maambukizi ya VVU wanakuwa na ufuasi mzuri wa dawa, kupunguza vifo
vya mama na mtoto, kupunguza maambukizi ya Malaria pamoja na kuongeza matumizi
ya huduma za uzazi wa mpango” alisema Ayubu.
=30=
No comments:
Post a Comment