Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Watekelezaji
wa mradi wa USAID Tulonge Afya wametakiwa kutumia fedha za utekelezaji kwa
mujibu wa taratibu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Kauli
hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu alipokuwa
akifungua kikao cha kuutambulisha mradi wa USAID Tulonge Afya kilichofanyika
katika ukumbi wa hoteli ya Gentle Hills iliyopo mjini Iringa jana.
Ayubu
alisema kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zinatolewa na serikili ya Marekani
kupitia shirika la maendeleo la Marekani USAID.
“Naomba fedha hizi zikatumike kwa kufuata utaratibu ili kufanikisha
kufikia malengo yake. Nataka niwakumbushe kuwa serikali ya awamu ya tano
imejipanga kikamilifu katika kusimamia na kufuatilia matumizi sahihi ya fedha
za wadau wa maendeleo na za serikali kwa lengo la kuhakikisha kuwa thamani ya
fedha kwenye miradi ya maendeleo inazingatiwa na watekelezaji” alisema
Ayubu.
Alisema
kuwa mradi huo unalenga kuhamasisha wanajamii kutumia huduma za afya
zinazotolewa kwenye vituo vya afya.
“Ninawahakikishia
kuwa serikali ya Mkoa itaendelea kushirikiana nanyi katika uboreshaji wa huduma
ili wananchi wakishahamasika waweze kwenda vituoni na kupata huduma zilizo bora”
alisema Ayubu.
=30=
No comments:
Post a Comment