Tuesday, November 6, 2012

RS IRINGA WASHAURIWA KUJIANDAA KABLA YA KUSTAAFU



Watumishi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa wameshauriwa kujiandaa mapema kabla ya kipindi cha kustaafu kufika ili kuondokana na msongo wa mawazo baada ya kustaafu.

Rai hiyo imetolewa na Afisa Elimu mstaafu Mkoa wa Iringa, Salum Maduhu wakati katika salamu zake za kuwaaga watumishi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika tafrija fupi ya kuwaaga watumishi waliostaafu na kuhamia katika vituo vipya vya kazi iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka akikabidhi zawadi kwa Salum Maduhu

Maduhu amesema “ndugu zangu watumishi lazima mjiandae mapema msisubiri ubaki mwaka mmoja wa kabla ya kustaafu ndiyo uanze kujiandaa anzeni mapema”. Amesema kuwa Serikali ni nzuri sana na pia inazotaratibu nzuri kwa watumishi wake wanaostaafu kwa kuwaandalia mafao yao baada ya muda wa utumishi wa Umma. Amesema pamoja na jambo hilo jema bado suala la kujiandaa kustaafu linabaki kwa mtumishi mwenyewe.

Wakati huohuo suala la watumishi kuongea elimu limefafanuliwa vizuri na aliyekuwa Msaidizi wa Mtendaji Mkuu, Onoria Ambrose. Amesema “wafanyakazi msome, pale wafanyakazi mnaposoma hasa wale wa kada za chini kipato kinaongezeka na pindi unapostaafu mafao nayo yanaongezeka”. Aidha, amewataka wafanyakazi kujiunga na kikundi cha kusaidiana na kukuza uchumi cha MSHIKAMANO kwa ajili ya kusaidiana.

Katika taarifa fupi ya Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Bibi. Gertrude Mpaka amesema kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imeandaa tafrija fupi ya kuwaaga watumishi waliostaafu katika utumishi wa Umma katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuwaaga watumishi waliohama na kuhamia vituo vingine vya kazi.

Kwa upande wa watumishi wastaafu, Mpaka amesema “ndugu wastaafu tumefanya kazi pamoja kwa muda mrefu sana, kwa upendo na ushirikiano mkubwa na kwa kufuata taratibu na kanuni zilizopo na weledi katika Utumishi wa Umma. Ushirikiano wenu ulisaidia Mkoa wetu kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa. Kwa msingi huo natumia fursa hii kuwashukuru kwa yale yote mazuri na utumishi uliotukuka mliyoyafanya katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kipindi chote tukiwa pamoja”.

Amesema “Sote tunatambua kwamba ninyi mlikuwa kiungo muhimu katika kufanikisha shughuli zote za Mkoa huu. Japo kuwa mmekwisha  kustaafu katika Utumishi wa Umma, bado ninyi ni nguzo muhimu sana katika mafanikio ya Mkoa wetu, tunaomba daima tuendelee kuwatumia katika ushauri na tunaamini kuwa ninyi ni hazina kubwa katika utendaji kazi kwa kuwa bado mnao uzoefu mkubwa ambao unahitajika katika kuendeleza Mkoa wetu wa Iringa” amesisitiza Mpaka.

Akiongelea watumishi waliohama, Katibu Tawala Mkoa wa Iringa amewakumbusha kipindi kilichopita cha utendaji kazi, na kusema “wote mtakumbuka kuwa katika kipindi chote mkiwa Watumishi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, tulifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa kwa lengo la kuupa mafanikio Mkoa wetu. Mtakumbuka pia kuwa kuna kipindi tulifanya kazi katika mazingira magumu yote ikiwa ni kuhakikisha shughuli za Serikali zinaendelea na kufanikiwa”. Ametoa wito kwa wafanyakazi hao kuwa nidhamu na uadilifu walivyokuwa navyo katika Mkoa wa Iringa wakaviendeleze huko walipohamia na kuwa mfano wa kuigwa kwa watumishi wengine.

Watumishi waliostaafu ni;
1.
Bibi. Zahara Kimela      
Msaidizi Mtendaji Mkuu
2.
Bw. Esau Sigalla
Mchumi Mkuu
3.
Bw. Agapiti Msimbe
Mpima Ardhi Mkuu
4.
Bw. Stanley Munisi
Afisa Wanyamapori Mkuu I
5.
Bw. Robert Kinyunyu
Mlinzi Mkuu
6.
Bw. Salum Maduhu
Afisa Elimu Mkuu
7.
Bw. Ephraim Mdegela
Mlinzi Mwandamizi
8.
Bw. Cletus Karigo
Daktari wa Mifugo Mkuu
9.
Bw. Vicent James
Katibu Tawala Msaidizi Miundo mbinu
10.
Bibi. Onoria Ambrose
Msaidizi wa Mtendaji Mkuu

Watumishi waliohama ni;
1.
Bw. Barnabas Ndunguru
DAP, Wizara ya Habari, Vijana,     Utamaduni na Michezo.

2.
Bw. Leornad Msigwa
Afisa Elimu Sekondari,
DED – Iringa
3.
Dkt. Ezekiel Mpuya
Mganga Mkuu wa Mkoa,
RAS Dodoma
4.
Bibi.  Grace Manga
Mhasibu Daraja la II
RAS Morogoro



TAFRIJA FUPI YA KUWAAGA WASTAAFU KATIKA OFISI YA MKUU WA MKOA NA WATUMISHI WALIOHAMIA KATIKA VITUO VIPYA VYA KAZI

 Mstaafu Zahara Kimela
 Mstaafu Onoria Mbrose
Mstaafu Ephrahim Mdelega 

Mstaafu Salum Maduhu 

Mstaafu Agapiti Msimbe  

Kingazi akimwaga maneno 

Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka akikabidhi zawadi kwa Onoria Ambrose.


 Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka akikabidhi zawadi kwa Ephraim Mdegela.
 
  Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka akikabidhi zawadi kwa Salum Maduhu.


 Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka akikabidhi zawadi kwa Salum Maduhu.


                                                                     Kicheko

Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka akikabidhi zawadi kwa Robert Kinyunyu.

 Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka akikabidhi zawadi kwa Robert Kinyunyu.
 
Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka akikabidhi zawadi kwa Zahara Kimela. 

Baadhi ya Wafanyakazi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa waliohudhuria hafla hiyo


Baadhi ya Wafanyakazi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa waliohudhuria hafla hiyo


Baadhi ya Wafanyakazi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa waliohudhuria hafla hiyo



Baadhi ya wastaafu waliohudhuria hafla hiyo


Baadhi ya wastaafu waliohudhuria hafla hiyo




Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka (katikati) akisoma taarifa fupi kuhusu watumishi waliostaafu utumishi wa Umma na watumishi waliohamia vituo vingine vya kazi. Kulia ni Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Utawala, Scolastica Mlawi na Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Mipango na Uratibu, Nuhu Mwasumilwe.

Wednesday, October 31, 2012




Aga Khan Health Services Resumes Delivery Services at Iringa Primary medical Center.
Aga Khan Health services Iringa has resumed delivery services and has registered its first delivery today morning.

Speaking with Daily news in an exclusive interview the Joining Hands Initiative project manager Anitah Muruve said that both the mother and the baby are in good condition. She said the delivery services have been established under Joining Hands: Improving Maternal, Newborn and Child Health (JHI) Project which is a Canadian International Development Agency (CIDA) funded initiative that aims to contribute to improved reproductive and maternal, newborn and child health (MNCH) in fifteen districts across five target regions in Tanzania.
 Kerstin Scheffler with her new new baby (cetre)

Kerstin Scheffler with her new new baby (cetre)

Maruve said that the project is focusing on improving quality of and access to maternal, newborn and child health services; increasing utilization of MNCH service at primary care level.

The project manager added that the project objectives are improving maternal, newborn and child health practices through behaviour change communication (BCC) and health promotion (HP)  and enhancing knowledge transfer and exchange on maternal, newborn and child health  through a strong public private partnership (PPP) approach under which the project is being implemented. The delivery services are open to the public. 

The Aga Khan Health Services Tanzania will continue to establish deliveries in its other health facilities in Mwanza, Dodoma, Mbeya and Morogoro regions.
Speaking on the services received, the mother of the new born baby Kerstin Scheffler said she has enjoyed and appreciate the services offered throughout she has been at the centre.

Veronica James, The Iringa Aga Khan hospital, Manager said her centre is keeping on improving her services in order to offer better health care services to the people. She further, calls upon people to go for better maternal and child health.

The project has got three phases as project implementation planning (PIP), inception and implementation.
=30=
MTOTO WA KWANZA AZALIWA HOSPITALI YA AGA KHAN-IRINGA


Hospitali ya Aga Khan imefanikia kuanzisha huduma ya kuboresha afya ya mama mjamzito na mtoto kwa kupitia mradi wake wa Tuunganishe mikono pamoja na mwanamke wa kwanza mjamzito amefanikiwa kujifungua salama asubuhi ya leo.

Baba mzazi wa mtoto aliyezaliwa leo hospitali ya Aga Khan Said Gallos Mlewa (kushoto) akiwa na familia yake.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kukabidhi zawadi kwa niaba ya jamuiya ya Aga Khan mkoa wa Iringa, Meneja wa hospitali ya Aga Khan-Iringa, Veronica James amesema “leo imekuwa ni siku ya furaha sana kwa hospitali ya Aga Khan na kwa wananchi wa manispaa ya Iringa na vitongoji vyake kutokana na huduma za kujifungua kwa mama mjamzito wa kwanza hospitalini hapa”.

Akielezea malengo ya mradi wa Tuunganishe nikono pamoja Veronica amesema kuwa mradi huo unalenga kuwasogezea wananchi huduma karibu na kwa ubora unaotakiwa kwa kupunguza foleni kwa wanawake wajawazito katika vituo vingine vinavyotoa huduma ya mama wajawazito na kujifungua kwa lengo la kuwapunguzia hadha wajawazito hao.

Meneja wa hospitali ya Aga Khan iringa amesema kuwa mradi huo unalenga kuongeza kiwango na matumizi ya huduma ya afya ya mama mjamzito na watoto nchini. Amesema kuwa mradi huo pia unalenga kuboresha kiwango cha upatikanaji wa huduma ya afya ya mama mjamzito na watoto. Malengo mengine ameyataja kuwa ni pamoja na kuboresha huduma ya afya yam ma mjamzito na watoto katika jamii na kushirikiana na kujifunza kuhusu afya ya mama mjamzito na watoto.

Akielezea furaha yake mama mzazi Kerstin Scheffler (38) amesema kuwa amefurahishwa na huduma katika hospitali hiyo kwa kipindi chote alichokuwa hospitalini hapo kutoka kwa madaktari na wauguzi. Mama huyo aliyejifungua mtoto wake wa tatu leo na kupewa jina la Malaika Lina ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuzitumia huduma za afya ya mama mjamzito na mtoto katika hospitali hiyo ili waweze kunufaika vizuri.
Katika maelezo yake ya jumla Daktari mfawidhi wa hospitali ya Aga Khan Iringa, Dkt. Jumaa Mbete amesema mama huyo amejifungua salama majira ya saa 3:25 asubuhi hospitali hapo na mtoto akiwa na uzito wa kilo 3.3.

Dkt. Mbete amesema kuwa lengo la hospitali yake ni kusaidiana na serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuimarisha huduma ya afya ya mama mjamzito na mtoto chini ya miaka mitano nchini.

Akiongelea gharama, Daktari mfawidhi amesema kuwa watu wengi wamekuwa wakihofia gharama katika hospitali yake jambo ambalo si kweli. Amesema kuwa gharama ni ndogo sana akitolea mfano wa gharama kwa mama mjamzito na watoto chini ya miaka mitano kuwa huduma ni bure. Amesema kuwa katika hospitali hiyo huduma hiyo hutolewa kwa masaa 24 na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza na kunufaika na huduma hiyo.

Mradi wa Tuunganishe mikono pamoja ni mradi wa miaka mitatu ukiendeshwa katika mikoa ya iringa, Dodoma, Mwanza, Mbeya na Morogoro na mashika yanayotekeleza mradi huo Mfuko wa Aga Khan, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, shirika la misaada ya maendeleo la Canada na chuo kikuu cha Aga Khan.

Wednesday, October 24, 2012


Obama and Romney in final push

 
Barack Obama (left) and Mitt Romney in Boca Raton, Florida 22 October 2012 
Europe did not get a mention in the third presidential debate on foreign policy

US President Barack Obama had the best lines, but perhaps Republican presidential challenger Mitt Romney had the best night.

Not in the sense that he won the debate - it was a draw if you have to judge these things that way.
But Mr Romney pivoted to President Peaceful and stomped on any suggestion he would take America into new foreign wars.
He didn't make any of the errors he had made in the past or say anything demonstrably silly. He said he would keep to Mr Obama's policy of withdrawing troops from Afghanistan by 2014 and agreed that sanctions against Iran were working. As one tweeter put it, his policy seemed to be "speak louder, and carry the same stick".
But Mr Obama was firm - and funny. He undermined Mr Romney's alarm that America had fewer ships than in 1916 by saying that it had fewer bayonets and horses as well. He said the 1980s were calling because they wanted their foreign policy back.
He didn't play the indignant and offended president, which I had expected him to do, but he did set out his achievements calmly and clearly.
Both men repeatedly tried to talk about the economy, which they know is of more concern to most Americans than what happens abroad.
The debate was depressing in that foreign policy seemed pretty much to equal the Middle East. Israel must have been mentioned dozens of times.
China got a brief look-in, in the last quarter of an hour, but mainly as a trade rival. I didn't hear Europe mentioned at all.
This final debate probably won't shift the opinion polls, but it saw a marked change in emphasis in Mr Romney's foreign policy.
That is a danger for him, in that it resurrects the old flip-flopping charge. But it also suggests a new confidence, that he has to convince people he is safe enough to entrust with the presidency.

From BBC NEWS

Tuesday, October 23, 2012

MKOA WA IRINGA WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA RUBADA




Mkuu wa Mkoa wa Iringa ametoa wito kwa viongozi wa mkoa wake kutoa ushirikiano wa kutosha kwa mamlaka ya uendelezaji wa bonde la mto Rufiji (RUBADA) ili kuwawezesha kuratibu na kusimamia vizuri mipango kabanbe ya kuendeleza shughuliza kilimo kwa ukanda wa kusini mwa Tanzania (SAGCOT).

Katika hotuba ya ufunguzi wa kikao cha viongozi na wataalamu wa mkoa wa Iringa kuhusu uendelezaji wa SAGCOT uliofanyika katika ukumbi wa VETA mjini Iringa iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Gerald Guninita kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma.

Mgeni rasmi Gerald Guninita ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo (katikati) akisoma hotuba wakati wa ufunguzi wa kikao cha viongozi na wataalamu wa mkoa wa Iringa kuhusu uendelezaji wa SAGCOT


wajumbe wa kikao cha viongozi na wataalamu wa mkoa wa Iringa kuhusu uendelezaji wa wa SAGCOT 


Amesema RUBADA imepewa majukumu ya kusimamia na kuratibu mipango ya SAGCOT ili malengo ya mipango hiyo yaweze kutekelezwa vizuri na kuinua hali ya wananchi nchini. Amesema katika kufanikisha hili RUBADA inatafuta na kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo chenye tija na viwanda kwa lengo la kuleta mapinduzi ya kijani. Amesema katika hilo RUBADA kwa kushirikiana na wilaya husika itaandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji ili maeneo ya uwekezaji yabainishwe na kutengwa kwa ajili ya wawekezaji watakayoyaendeleza pamoja na wakulima wadogo wadogo wanaoyazunguka maeneo ya miradi hiyo.

Guninita amesema kwa kuzingatia kazi nzuri inayofanywa na RUBADA katika kutekeleza mipango hiyo, ushirikiano wa viongozi na wataalamu hao ni chachu katika ufanikishaji wa malengo hayo. Ameelezea matarajio yake kwa viongozi na wataalamu hao baada ya kikao hicho kuwa watakuwa mabalozi wazuri wa kuwaelimisha wananchi katika maeneo yao ili wawe washiriki wazuri katika kutekeleza mpango huo.

Akiwasilisha mpango wa SAGCOT Mkurugenzi Mkuu wa uendeshaji wa bonde la Rufiji, Aloyce Masanja amesema kuwa hakuna nchi iliyofanikiwa duniani kuichumi na kuondokana na umasikini pasipo mapinduzi ya kilimo na viwanda. Akiongelea takwimu, amesema kuwa asilimia 65 ya malighafi za viwanda zinatokana na kilimo wakati asilimia zaidi ya 55 ya mfumuko wa bei huchangiwa na mazao ya kilimo. Amesema katika hekta milioni 44 zinazofaa kwa kilimo ni asilimia 23 pekee ndiyo zimetumika.
Akiongelea tofauti kati ya kilimo kwanza na sera nyingine zilizopita, Masanja amesema kuwa mipango na jitihada za zamani ziliibuliwa, kupangwa na kutekelezwa na serikali na mashirika yake pasipo kuwahusisha wadau wengine kikamilifu. Amesema tofauti na mipango ya awali kilimo kwanza ni mtazamo mpana wa mabadiliko ya kisekta na uzoefu uliopatikana kutokana na mipango iliyotekelezwa hapo awali na sasa kilimo kwanza kimeshirikisha wadau wote.   

Mkurugenzi Mkuu wa uendeshaji wa bonde la Rufiji ameyataja malengo ya SAGCOT kuwa ni kutatua matatizo yanayoikabili sekta ya kilimo hasa upatikanaji wa mitaji, vyama vya wakulima, miundombinu ya kilimo, uharibifu wa mazingira, ukosefu wa masoko, uwekezaji mdogo katika kilimo na uboreshaji wa sera zinazohusu kilimo. Amesema malengo mengine ni kuwahamasisha wakulima wadogo na kuwaunganisha katika vikundi na kuwafanya walime kilimo cha kibiashara.

Masanja amesema kuwa RUBADA imekuwa pia ikiwapa kipaumbele vijana katika shughuli mbalimbali za kujiongezea kipato. Amesema “kila tunapoanzisha miradi ya RUBADA tunakuwa tukianzisha kambi za vijana ambapo tunawafundisha mbinu bora za kilimo na matumizi ya dhana za kilimo” amesisitiza Masanja.

=30=









Sunday, October 7, 2012

MAONESHO YA ASALI DAR














SENJE AHIMIZA VIFUNGASHIO KATIKA BIDHAA





Halmashauri nchini zimeshauriwa kulipa kipaumbele suala la vifungashio katika mazao ya nyuki ili kutoa taarifa sahihi kwa mlaji.

Ushauri huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Immaculte Senje alipokuwa alitoa tathmini yake juu ya changamoto wanazokabiliana nazo katika kufikisha asali sokoni muda mfupi baada ya kutembelea mabanda ya Halmashauri katika maonesho ya kitaifa ya mazao ya nyuki yajulikanayo kama ‘Dar es Salaam Honey Exhibition’ yanayoendelea katika uwanja wa maonesho ya biashara ya Mwl. Julius Nyerere, barabara ya kilwa.

Senje amesema kuwa mabanda mengi aliyotembelea yanakabiliwa na changamoto ya vifungashio. Amesema “nadhani umefika wakati kwa Halmashauri zetu kulipa uzito suala la vifungashio katika mazao ya nyuki ili kuweza kuendana na uhalisia wa soko”. Amesema umuhimu wa vifungashio katika mazao ya nyuki hasa asali, unamuwezesha mlaji kupata taarifa kamili juu ya bidhaa anayoitumia na kiwango cha ubora wake.
Afisa Uhusiano wa Idara ya Uhamiaji Makao Makuu, Al-Haji M. Batenga alipotembelea banda la Manispaa ya Iringa katika Maonesho ya Asali

Mjasiliamali Msafiri Chengula kutoka kikundi cha Anamed chenye mizinga zaidi ya 200 katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa amesema kuwa changamoto wanayoipata ni uuzaji asali kwa njia ya lejaleja, jambo linalowasababishia tatizo katika kuhifadhi fedha na kuzipangia matumizi sababu fedha hizo hazikai. Amesema kuwa uchomaji misiti umekuwa ukiathili sana utengenezaji wa asali sababu nyuki wamekuwa wakikimbia au kuungua. Changamoto nyingine ameitaja kuwa ni tabia ya wizi wa asali katika kipindi cha uvunaji ambacho kwa wilaya ya Iringa amekitaja kuwa ni kati ya miezi ya Mei hadi Julai kutokana na ukame hali inayowalazimisha walinaji kuhamia msituni wakati huo.

Changamoto ya vifungashio pia linaikumba Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa mujibu wa Afisa Misitu wa Msaidizi, Enock Changime, amesema “sehemu ya kuhifadhia asili asali ili iweze kuingia sokoni kwa maana ya vifungashio ni tatizo kwa sababu vifungshio vingi vinatoka nchi ya Kenya”.

Changime amesema kuwa changomoto nyingine ni udogo wa mwamko wa jamii katika suala la ufugaji nyuki. Amesema manispaa ya Iringa imekuwa ikihamasisha  jamii kujiunga katika vikundi na kuvipa mafunzo juu ya ufugaji nyuki sambamba na na misaada ya mizinga ya kuanzia ufugaji huo. 

Amesema kutikana na changamoto ya uhaba wa wataalamu, Manispaa ya Iringa imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na sna na Halmashauri ya wilaya ya Iringa katika kuunganisha nguvu ya rasilimali wataalamu ili kuweza kukuza sekta ya nyuki katika halmashauri hizo.

Akiongelea umuhimu wa vifungashio katika kukuza soko la bidhaa nchini, Kaimu Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka Wakala wa Vipimo nchini Irene John amesema ili bidhaa iweze kutambulika ndani na nje ya nchi suala la vifungishio sahihi ni muhimu sana. Amesema kuwa ni vema kuyapa uzito unaoshahili mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa ufungashaji bidhaa za mazao ya nyuki, ameyataja mambo hayo kuwa ni masharti kuwa ni kuandika maelezo na kiasi cha ufungashaji. Mengine ameyataja kuwa ni uzuiaji wa ufungashaji wenye udanganyifu na uthibiti wa vipimo.

Maonesho ya kitaifa ya mazao ya nyuki yalianza katika uwanja wa maonesho ya biashara wa Mwl. Julius Nyerere tarehe 4-7 Oktoba, 2012 na yalitanguliwa na kongamano la kitaifa la wadau wa sekya ya asali kutokana na agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda.
=30=

Tuesday, September 25, 2012

IRINGA TUMIENI FURSA YA UTALII




Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma amewataka wananchi wa mkoa huo kutumia fursa ya maadhimisho ya siku ya utalii duniani yanayofanyika kimkoa katika manispaa ya Iringa kutembelea maonesho hayo na kushiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo ili kuweza kupata elimu na taarifa z utalii.

Wito huo ameutoa katika hotuba yake ya ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya utalii duniani yanayofanyika kimkoa katika uwanja wa Samora, Manispaa ya Iringa.   
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma (wa kwanza kulia) akiwa katika moja ya mapango ya kihistoria katika kuhamasisha utalii wa ndani.

Dkt. Christine amesema “natoa wito kwa wananchi wote kutumia fursa hii kutembelea maonesho na kushiriki  katika shughuli mbalimbali za maadhimisho haya”.

Amesema maonesho hayo yatatoa fursa ya kufahamiana na kupanua wigo wa kufanya biashara za utalii. Amesema kuwa maadhimisho yatahusisha maonesho ya bidhaa na shughuli mbalimbali za kitalii, michezo, kutembelea vivutio vya kitalii vilivyopo mkoani Iringa na kutoa elimu kuhusu uendeshaji wa biashara za utalii.

Akielezea madhumuni ya maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa amesema kuwa madhumuni ya maadhimisho hayo ni Kutoa umuhimu wa sekta ya utalii kwa maendeleo ya mwanadamu katika nyanja mbalimbali. Amezitaja nyanza hizo kuwa ni pamoja na utamaduni, uchumi, mazingira pamoja na nyingine.

Dkt. Christine amesema kuwa matokeo ya maadhimisho hayo hayawezi kuonekana kwa muda mfupi kwa sababu ni suala linalohitaji hamasa ya muda mrefu. Ameelezea matumaini yake kuwa Mkoa wa Iringa utazidi kuendeleza kwa kasi iliyopo, ukuaji wa utalii na hatimae wananchi kunufaika na utalii huo.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa amesema kuwa mkoa wake umejaaliwa kuwa na vivutio Vinci vya utalii ambavyo bado havijafahamika sana kwa wananchi na wadau wengine. Amevitaja vivutio vilivyopo kuwa ni pamoja na mila na desturi za watu wa ukanda huo, maeneo ya hifadhi za mimea na wanyama, mandhari nzuri na za kuvutia, maeneo ya kilimo, maporomoko ya maji na maeneo ya kihistoria.

Nae mwenyekiti wa Kamati ya kuendeleza utalii kwa mkoa wa Iringa ambae pia ni katibu Tawala msaidizi, Sehemu ya Uchumi na Sekta za Uzalishaji, Adam Swai amesema kuwa malengo mahususi ya kufanya maadhimisho katika manispaa ya Iringa ni kuhamasisha wadau mbalimbali kutambua umuhimu wa sekta ya utalii katika kujiletea maendeleo. Ameyataja maadhimisho hayo kuwa ni chachu ya kuendeleza sekta ya utalii katika ukanda wa Kusini ili wananchi waweze kufaidika na utalii huo.

Ikumbukwe kuwa Mkoa wa Iringa ulitangazwa na serikali kuwa kutovu cha kuendeleza utalii kwa Ukanda wa kusini mwaka 2009. aidha, maadhimisho hayo yatafanyika kwa siku tatu, kuanzia tarehe 25 hadi 27 Septemba 2012.
=30=