Saturday, November 17, 2012

RC AKEMEA UKWEPAJI KODI


Mkuu wa Mkoa wa Iringa amewataka wananchi kuachana na tabia ya kukwepa kulipa kodi na kuwa wazalendo kwa mkoa wao na Taifa lao kwa ujumla wakati akikemea tabia ya wafanyabiashara wanaokwepa kutumia mashine za kieletroni za kutolea risiti.


Mkuu wa Mkoa amesema hayo katika hotuba yake kwenye maadhimisho ya siku ya mlipakodi iliyofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria tawi la Iringa iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dkt. Leticia Warioba.

Dkt. Warioba amesema “bado wapo walipakodi ambao sio wazalendo.Walipakodi ambao mpaka sasa wanakwepa kodi. Tabia hii ya kukwepa kodi siyo ya kizalendo na ningependa kuwaasa muiache mara moja”. Amesema kuwa ukadiliaji na ukusanyaji wa kodi vinafanyika kwa mujibu wa sheria za kodi na ni muhimu kwa kila mlipa kodi kuheshimu sheria na taratibu nchi ilizojiwekea.

Amesema tabia ya kukwepa kodi imekuwa ikiwafanya wafanyabiashara kupitisha bidhaa vichochoroni badala ya kupitisha bidhaa hizo kwenye ofisi za forodha zilizopo mipakani. Amesema kuwa utaratibu huo unafanyika kinyume na sheria za nchi na kutaka tabia hiyo iachwe mara moja.

Akiongelea matumizi ya mashine ya kieletroniki za kutolea risiti, Dkt. Leticia amesema “matumizi ya mashine hizo ni changamoto katika utendaji kazi wa Mamlaka ya Mapato nchini, ningependa kuwafahamisha kuwa, matumizi ya mashine hizi ni agizo la Serikali na lengo lake ni kuhakikisha kodi ya ongezeko la thamani inakusanywa ipasanyo”.

Amewataka wale wote waliosajiliwa na kodi ya ongezeko la thamani kutumia mashine za kieletroniki za kutolea risiti kwa kila mauzo wanayofanya. Amesema kuwa mashine hizo zinatumika kwa mujibu wa sheria ya bunge hivyo utekelezaji wake ni lazima.

Wakati huohuo, Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Iringa imefanikiwa kuvuka lengo kwa kukusanya zaidi ya asilimia 100 ya lengo iliyowekewa la idara ya ushuru wa forodha na kodi za ndani. Katika maelezo ya Meneja wa mamlaka ya mapata Mkoa wa Iringa, Rozalia Mwenda amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2011/2012 Mkoa wa Iringa ulipangiwa kukusanya jumla ya shilingi  23,761,800,000/= lengo la idara ya ushuru wa forodha likiwa shilingi 110,100,000/= na lengo la idara ya kodi za ndani likiwa shilingi 23,651,700,000/=. Amesema kwa kipindi hicho Mkoa ulikusanya shilingi 24,730,752,185 sawa na asilimia 105 ya utendaji.

Akiongelea ubora wa huduma kwa wateja, Rozalia amesema “mamlaka ya mapato makao makuu, mikoani hadi wilayani, inatekeleza sera ya ubora ambayo inaelekeza utendaji kazi wenye lengo la kutoa huduma bora inayokidhi na hata kupita matarajio ya mteja”. Amesema “baada ya kufanyika  kwa ukaguzi wa ubora wa huduma zetu na kampuni ya wakaguzi wa nje, mamlaka ilitunukiwa cheti cha kimataifa cha ubora wa viwango cha ISO 9001:2008”. Amesema kuwa mamlaka yake imepanga kutathmini mara kwa mara viwango vya huduma tunazotoa kwa walipa kodi ili kuhakikisha kuwa mahitaji ya walipakodi yanazingatiwa katika mipango ya mamlaka ya kimkakati.

Amesema kuwa mamlaka yake inaendeleza ushirikiano baina yake na mlipakodi kwa lengo la kudumisha ushirikiano wa kulipa kodi kwa mujibu wa sheria kwa kutoa huduma bora. Amesisitiza kuwa urafiki baina mamlaka na mlipakodi sharti uongeze tija katika kukusanya mapato ya Serikali kwa lengo la kutokumuumiza mlipa kodi na wala Serikali.

Meneja wa mamlaka ya mapato mkoa wa Iringa ameahidi kuongeza juhudi katika utendaji kazi, amesema “mimi na wafanyakazi  wa mamlaka ya mapato Mkoa wa Iringa tunaahidi kuongeza, juhudi, maarifa na uadilifu katika kuhakikisha tunavuka malengo tuliyopangiwa kama tulivyokwishaonesha kipindi kilichopita. Kwa mshikamano na mikakati tuliyonayo, tunaamini malengo ya mwaka 2012/2013 ambayo ni shilingi 33.4 bilioni yanafikiwa”.

Wiki ya maadhimisho ya 6 ya sherehe ya mlipakodi kitaifa ilianza tarehe 01-07 Novemba, 20122 ikiongozwa na kaulimbiu isemayo “ulipaji kodi wa hiari Kwa Taifa lenye mafanikio” ikiwa na lengo kuu la kuboresha huduma kwa mlipakodi.
=30=



MKOA WA IRINGA WAZIDI KUFANIKIWA KATIKA SEKTA YA KILIMO
Mkoa wa Iringa umeendelea kupata mafanikio makubwa katika Sekta ya Uchumi na Uzalishaji mali kwa kuongeza matumizi ya zana za kilimo hadi kufikia asilimia 15 kwa wakazi wa Mkoa huo.

 Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Scolastica Mlawi akifafanua jambo.

Mafanikio hayo yameelezwa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Scolastica Mlawi wakati akifungua kikao cha siku mbili cha kupitia taarifa za uekelezaji wa kazi za Sehemu ya uchumi na sekta za uzalishaji na kuainisha vipaumbele kwa mkoa wa Iringa kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

Scolastica amesema “mafanikio kwa upande wa sekta ya kilimo ni pamoja na ongezeko la matumizi ya zana za kilimo ambapo kwa sasa asilimia 15 ya wakazi wa mkoa huu wanatumia matrekta makubwa na madogo katika Kilimo”. Amesema asilimia 20 ya wakazi wanatumia wanyamakazi na asilimia 65 wanatumia jembe la mkono ikilinganishwa na asilimia 75 ya wakulima waliokuwa wanatumia jembe la mkono mwaka 2005.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa amesema kuwa pato la mkoa wa Iringa limeongezeka toka Sh. 867,482 mwaka 2005 hadi kufikia Sh. 1,985,708 mwaka 2011, wakati pato la mkazi mwaka 2005 lilikuwa Sh. 558,444 na limeongezeka hadi kufikia Sh. 1,125,503 mwaka 2011.
Akiongelea maandalizi ya kilimo msimu huu, amesema kuwa msimu wa kilimo umeanza na wakulima wameonesha jitihada kubwa katika kulima na kupanda mazao mbalimbali ya chakula na biashara.

Amesema “msimu huu tunajipanga zaidi katika kuhimiza mazao yanayostahimili ukame kama vile alizeti, mtama, muhogo na viazi vitamu. Kwa pamoja tuhimize kilimo cha mazao haya katika maeneo yote yenye ukame (upungufu wa mvua) katika wilaya zote hasa wilaya ya Iringa (Tarafa ya Idodi, Isimani na Pawaga), wilaya ya Kilolo (Tarafa ya Mahenge na Mazombe) wilaya ya Mufindi (Tarafa ya Sadani na Malangali)”.

Akiongelea ufanisi wa kilimo Scolastica amesema “ili kilimo chetu kiweze kufanikiwa vizuri tunahitaji kuwaelimisha wakulima wetu mbinu bora za kilimo ikiwemo matumizi bora na sahihi ya pembejeo za Kilimo”.

Awali Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Sekta ya Uchumi na Uzalishaji, Adam Swai alisema kuwa lengo la kikao hicho ni kutoa taarifa za utekelezaji wa kazi kutoka katika Halmashauri za wilaya ili kujadili tathamini, matokeo na kubadilishana uzoefu wa shughuli na kutoa ushauri wa pamoja katika  kuboresha utekelezaji wa shughuli na kupata takwimu halisia katika sekta ya uchumi. Aidha, amesema kuwa kikao hicho kitasaidia katika kuandaa taarifa ya Mkoa itakayoonyesha vipaumbele vichache ambavyo vitaleta matokeo na mafanikio.
=30=

Sunday, November 11, 2012

MATUKIO YA KUKABIDHI KIKOMBE CHA MSHINDI WA PILI WANAWAKE KUVUTA KAMBA A

 Kombe la mshindi wa pili kuvuta kamba wanawake

 Nahodha wa timu Agnes Mlula akimkabidhi kombe mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka

 Kaimu Mwenyekiti mstaafu wa Klabu ya Shimiwi Ras Iringa Gillian Bukori akimkabidhi cheti cha ushiriki wa Mkoa mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Gertrude Mpaka.





 Baadhi wa wachezaji wa timu hiyo ya kuvuta kamba wanawake




  




 Picha ya pajama baina ya wachezaji, viongozi wa Mkoa na mgeni rasmi.

Wakati wa Burudani



RAS IRINGA AKABIDHIWA KOKOMBE CHA SHIMIWI




Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Getrude K. Mpaka ameishauri Wizara ya Fedha kuangalia uwezekano wa kuongeza wigo wa fedha katika bajeti za Mikoa ili kuweza kuiwezesha mikoa kushiriki kikamilifu katika michezo ya shirikisho la michezo kwa Wizara na Idara za Serikli (SHIMIWI).

Ushauri huo ameutoa katika hafla fupi ya kukabidhiwa kikombe na kuipongeza timu ya kuvuta kamba wanawake ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa baada ya kuibuka mshindi wa pili nyuma ya timu ya Ikulu kwa mchezo wa kuvuta kamba wanawake kutoka klabu ya Ras Iringa iliyoshiriki katika mashindano hayo mjini Morogoro.
 Nahodha wa timu Agnes Mlula (kulia) akimkabidhi kombe mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka

Mpaka amesema “ni vizuri Wizara ya Fedha iangalie jinsi ya kuongeza ceiling kwa Mikoa ili watumishi wetu waweze kushiriki kikamilifu kama watumishi wa timu za Wizara na kutokujiona ni wanyonge”. Amesema kuwa mwakani Ofisi yake itajipanga vizuri zaidi ili iweze kupeleka timu kubwa zaidi ya wachezaji wengi katika michezo tofauti tofauti. 

Ameitaka timu hiyo kutobweteka na kuendelea na mazoezi makali ili mwakani iweze kuibuka mshindi wa kwanza. Katika kufanikisha hilo amemuagiza Afisa Michezo Mkoa wa Iringa, Kenneth Komba kuhakikisha anaandaa mabonanza ya michezo mengi ili kuweza kupata wanamichezo mahiri watakaouletea Mkoa sifa kubwa zaidi.
Akielezea mafanikio ya timu hiyo Kaimu Mwenyekiti mstaafu wa Klabu SHIMIWI RAS Iringa, Gillian Bukori amesema kuwa timu hiyo iliondoka Mkoani hapa tarehe 20/09/2012 baada ya kuagwa na Katibu Tawala Mkoa wa Iringa na kuitaka timu hiyo irudi na kikombe cha ushindi. 

Bukori amesema kuwa mafanikio hayo ni kutokana na ushiriki binafsi wa Katibu Tawala Mkoa, Getrude Mpaka, Uongozi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na watumishi wote. Amesema kuwa ushindi huo umechangiwa na mshikamano, upendo na kujituma kwa mtu mmoja mmoja ndani ya timu. 

Amesema matarajio ya timu hiyo ni mwakani kuibuka na ushindi wa kwanza na kuutaka uongozi ulioingia madarakani awamu hii kuendeleza upendo na mshikamano ili kuleta mafanikio makubwa zaidi katika Mkoa.

Akitoa neno la shukrani, Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Menejimenti ya Serikali za Mitaa, Wamoja Ayubu amesema kuwa Mkoa utaendelea kuomba wigo kuongezwa katika bajeti ili kuiwezesha timu ya Mkoa kushiriki kikamilifu katika michezo hiyo. Amesema Mkoa utakuwa bega kwa bega na timu hiyo ili iendelee kufanya vizuri katika mashindano hayo. 

Akiongelea mazoezi, Ayubu amesema kuwa mazoezi ni jambo la muhimu sana si kwa mwanamichezo tu, bali kwa kila mtumishi na wakati wote ni muafaka kwa kufanya mazoezi si mpaka wakati wa michezo pekee. 

Wamoja ambaye pia ni mchezi mahiri wa mchezo wa pete amesema kuwa ili timu hiyo iendelee kuwa juu suala la kujituma ni la muhimu sana.

Timu ya kuvuta kamba wanawake ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa iliibuka mshindi wa pili katika mashindano hayo kitaifa yaliyofanyika Morogoro ikiwa ni hatua nzuri zaidi ikilinganishwa na mwaka uliotangulia ilipoibuka mshindi wa nne.

 Kaimu Mwenyekiti mstaafu wa Klabu ya Shimiwi Ras Iringa Gillian Bukori akimkabidhi cheti cha ushiriki wa Mkoa mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Gertrude Mpaka.




=30=

Tuesday, November 6, 2012

RS IRINGA WASHAURIWA KUJIANDAA KABLA YA KUSTAAFU



Watumishi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa wameshauriwa kujiandaa mapema kabla ya kipindi cha kustaafu kufika ili kuondokana na msongo wa mawazo baada ya kustaafu.

Rai hiyo imetolewa na Afisa Elimu mstaafu Mkoa wa Iringa, Salum Maduhu wakati katika salamu zake za kuwaaga watumishi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika tafrija fupi ya kuwaaga watumishi waliostaafu na kuhamia katika vituo vipya vya kazi iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka akikabidhi zawadi kwa Salum Maduhu

Maduhu amesema “ndugu zangu watumishi lazima mjiandae mapema msisubiri ubaki mwaka mmoja wa kabla ya kustaafu ndiyo uanze kujiandaa anzeni mapema”. Amesema kuwa Serikali ni nzuri sana na pia inazotaratibu nzuri kwa watumishi wake wanaostaafu kwa kuwaandalia mafao yao baada ya muda wa utumishi wa Umma. Amesema pamoja na jambo hilo jema bado suala la kujiandaa kustaafu linabaki kwa mtumishi mwenyewe.

Wakati huohuo suala la watumishi kuongea elimu limefafanuliwa vizuri na aliyekuwa Msaidizi wa Mtendaji Mkuu, Onoria Ambrose. Amesema “wafanyakazi msome, pale wafanyakazi mnaposoma hasa wale wa kada za chini kipato kinaongezeka na pindi unapostaafu mafao nayo yanaongezeka”. Aidha, amewataka wafanyakazi kujiunga na kikundi cha kusaidiana na kukuza uchumi cha MSHIKAMANO kwa ajili ya kusaidiana.

Katika taarifa fupi ya Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Bibi. Gertrude Mpaka amesema kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imeandaa tafrija fupi ya kuwaaga watumishi waliostaafu katika utumishi wa Umma katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuwaaga watumishi waliohama na kuhamia vituo vingine vya kazi.

Kwa upande wa watumishi wastaafu, Mpaka amesema “ndugu wastaafu tumefanya kazi pamoja kwa muda mrefu sana, kwa upendo na ushirikiano mkubwa na kwa kufuata taratibu na kanuni zilizopo na weledi katika Utumishi wa Umma. Ushirikiano wenu ulisaidia Mkoa wetu kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa. Kwa msingi huo natumia fursa hii kuwashukuru kwa yale yote mazuri na utumishi uliotukuka mliyoyafanya katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kipindi chote tukiwa pamoja”.

Amesema “Sote tunatambua kwamba ninyi mlikuwa kiungo muhimu katika kufanikisha shughuli zote za Mkoa huu. Japo kuwa mmekwisha  kustaafu katika Utumishi wa Umma, bado ninyi ni nguzo muhimu sana katika mafanikio ya Mkoa wetu, tunaomba daima tuendelee kuwatumia katika ushauri na tunaamini kuwa ninyi ni hazina kubwa katika utendaji kazi kwa kuwa bado mnao uzoefu mkubwa ambao unahitajika katika kuendeleza Mkoa wetu wa Iringa” amesisitiza Mpaka.

Akiongelea watumishi waliohama, Katibu Tawala Mkoa wa Iringa amewakumbusha kipindi kilichopita cha utendaji kazi, na kusema “wote mtakumbuka kuwa katika kipindi chote mkiwa Watumishi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, tulifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa kwa lengo la kuupa mafanikio Mkoa wetu. Mtakumbuka pia kuwa kuna kipindi tulifanya kazi katika mazingira magumu yote ikiwa ni kuhakikisha shughuli za Serikali zinaendelea na kufanikiwa”. Ametoa wito kwa wafanyakazi hao kuwa nidhamu na uadilifu walivyokuwa navyo katika Mkoa wa Iringa wakaviendeleze huko walipohamia na kuwa mfano wa kuigwa kwa watumishi wengine.

Watumishi waliostaafu ni;
1.
Bibi. Zahara Kimela      
Msaidizi Mtendaji Mkuu
2.
Bw. Esau Sigalla
Mchumi Mkuu
3.
Bw. Agapiti Msimbe
Mpima Ardhi Mkuu
4.
Bw. Stanley Munisi
Afisa Wanyamapori Mkuu I
5.
Bw. Robert Kinyunyu
Mlinzi Mkuu
6.
Bw. Salum Maduhu
Afisa Elimu Mkuu
7.
Bw. Ephraim Mdegela
Mlinzi Mwandamizi
8.
Bw. Cletus Karigo
Daktari wa Mifugo Mkuu
9.
Bw. Vicent James
Katibu Tawala Msaidizi Miundo mbinu
10.
Bibi. Onoria Ambrose
Msaidizi wa Mtendaji Mkuu

Watumishi waliohama ni;
1.
Bw. Barnabas Ndunguru
DAP, Wizara ya Habari, Vijana,     Utamaduni na Michezo.

2.
Bw. Leornad Msigwa
Afisa Elimu Sekondari,
DED – Iringa
3.
Dkt. Ezekiel Mpuya
Mganga Mkuu wa Mkoa,
RAS Dodoma
4.
Bibi.  Grace Manga
Mhasibu Daraja la II
RAS Morogoro



TAFRIJA FUPI YA KUWAAGA WASTAAFU KATIKA OFISI YA MKUU WA MKOA NA WATUMISHI WALIOHAMIA KATIKA VITUO VIPYA VYA KAZI

 Mstaafu Zahara Kimela
 Mstaafu Onoria Mbrose
Mstaafu Ephrahim Mdelega 

Mstaafu Salum Maduhu 

Mstaafu Agapiti Msimbe  

Kingazi akimwaga maneno 

Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka akikabidhi zawadi kwa Onoria Ambrose.


 Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka akikabidhi zawadi kwa Ephraim Mdegela.
 
  Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka akikabidhi zawadi kwa Salum Maduhu.


 Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka akikabidhi zawadi kwa Salum Maduhu.


                                                                     Kicheko

Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka akikabidhi zawadi kwa Robert Kinyunyu.

 Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka akikabidhi zawadi kwa Robert Kinyunyu.
 
Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka akikabidhi zawadi kwa Zahara Kimela. 

Baadhi ya Wafanyakazi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa waliohudhuria hafla hiyo


Baadhi ya Wafanyakazi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa waliohudhuria hafla hiyo


Baadhi ya Wafanyakazi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa waliohudhuria hafla hiyo



Baadhi ya wastaafu waliohudhuria hafla hiyo


Baadhi ya wastaafu waliohudhuria hafla hiyo




Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka (katikati) akisoma taarifa fupi kuhusu watumishi waliostaafu utumishi wa Umma na watumishi waliohamia vituo vingine vya kazi. Kulia ni Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Utawala, Scolastica Mlawi na Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Mipango na Uratibu, Nuhu Mwasumilwe.

Wednesday, October 31, 2012




Aga Khan Health Services Resumes Delivery Services at Iringa Primary medical Center.
Aga Khan Health services Iringa has resumed delivery services and has registered its first delivery today morning.

Speaking with Daily news in an exclusive interview the Joining Hands Initiative project manager Anitah Muruve said that both the mother and the baby are in good condition. She said the delivery services have been established under Joining Hands: Improving Maternal, Newborn and Child Health (JHI) Project which is a Canadian International Development Agency (CIDA) funded initiative that aims to contribute to improved reproductive and maternal, newborn and child health (MNCH) in fifteen districts across five target regions in Tanzania.
 Kerstin Scheffler with her new new baby (cetre)

Kerstin Scheffler with her new new baby (cetre)

Maruve said that the project is focusing on improving quality of and access to maternal, newborn and child health services; increasing utilization of MNCH service at primary care level.

The project manager added that the project objectives are improving maternal, newborn and child health practices through behaviour change communication (BCC) and health promotion (HP)  and enhancing knowledge transfer and exchange on maternal, newborn and child health  through a strong public private partnership (PPP) approach under which the project is being implemented. The delivery services are open to the public. 

The Aga Khan Health Services Tanzania will continue to establish deliveries in its other health facilities in Mwanza, Dodoma, Mbeya and Morogoro regions.
Speaking on the services received, the mother of the new born baby Kerstin Scheffler said she has enjoyed and appreciate the services offered throughout she has been at the centre.

Veronica James, The Iringa Aga Khan hospital, Manager said her centre is keeping on improving her services in order to offer better health care services to the people. She further, calls upon people to go for better maternal and child health.

The project has got three phases as project implementation planning (PIP), inception and implementation.
=30=
MTOTO WA KWANZA AZALIWA HOSPITALI YA AGA KHAN-IRINGA


Hospitali ya Aga Khan imefanikia kuanzisha huduma ya kuboresha afya ya mama mjamzito na mtoto kwa kupitia mradi wake wa Tuunganishe mikono pamoja na mwanamke wa kwanza mjamzito amefanikiwa kujifungua salama asubuhi ya leo.

Baba mzazi wa mtoto aliyezaliwa leo hospitali ya Aga Khan Said Gallos Mlewa (kushoto) akiwa na familia yake.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kukabidhi zawadi kwa niaba ya jamuiya ya Aga Khan mkoa wa Iringa, Meneja wa hospitali ya Aga Khan-Iringa, Veronica James amesema “leo imekuwa ni siku ya furaha sana kwa hospitali ya Aga Khan na kwa wananchi wa manispaa ya Iringa na vitongoji vyake kutokana na huduma za kujifungua kwa mama mjamzito wa kwanza hospitalini hapa”.

Akielezea malengo ya mradi wa Tuunganishe nikono pamoja Veronica amesema kuwa mradi huo unalenga kuwasogezea wananchi huduma karibu na kwa ubora unaotakiwa kwa kupunguza foleni kwa wanawake wajawazito katika vituo vingine vinavyotoa huduma ya mama wajawazito na kujifungua kwa lengo la kuwapunguzia hadha wajawazito hao.

Meneja wa hospitali ya Aga Khan iringa amesema kuwa mradi huo unalenga kuongeza kiwango na matumizi ya huduma ya afya ya mama mjamzito na watoto nchini. Amesema kuwa mradi huo pia unalenga kuboresha kiwango cha upatikanaji wa huduma ya afya ya mama mjamzito na watoto. Malengo mengine ameyataja kuwa ni pamoja na kuboresha huduma ya afya yam ma mjamzito na watoto katika jamii na kushirikiana na kujifunza kuhusu afya ya mama mjamzito na watoto.

Akielezea furaha yake mama mzazi Kerstin Scheffler (38) amesema kuwa amefurahishwa na huduma katika hospitali hiyo kwa kipindi chote alichokuwa hospitalini hapo kutoka kwa madaktari na wauguzi. Mama huyo aliyejifungua mtoto wake wa tatu leo na kupewa jina la Malaika Lina ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuzitumia huduma za afya ya mama mjamzito na mtoto katika hospitali hiyo ili waweze kunufaika vizuri.
Katika maelezo yake ya jumla Daktari mfawidhi wa hospitali ya Aga Khan Iringa, Dkt. Jumaa Mbete amesema mama huyo amejifungua salama majira ya saa 3:25 asubuhi hospitali hapo na mtoto akiwa na uzito wa kilo 3.3.

Dkt. Mbete amesema kuwa lengo la hospitali yake ni kusaidiana na serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuimarisha huduma ya afya ya mama mjamzito na mtoto chini ya miaka mitano nchini.

Akiongelea gharama, Daktari mfawidhi amesema kuwa watu wengi wamekuwa wakihofia gharama katika hospitali yake jambo ambalo si kweli. Amesema kuwa gharama ni ndogo sana akitolea mfano wa gharama kwa mama mjamzito na watoto chini ya miaka mitano kuwa huduma ni bure. Amesema kuwa katika hospitali hiyo huduma hiyo hutolewa kwa masaa 24 na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza na kunufaika na huduma hiyo.

Mradi wa Tuunganishe mikono pamoja ni mradi wa miaka mitatu ukiendeshwa katika mikoa ya iringa, Dodoma, Mwanza, Mbeya na Morogoro na mashika yanayotekeleza mradi huo Mfuko wa Aga Khan, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, shirika la misaada ya maendeleo la Canada na chuo kikuu cha Aga Khan.