Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Mkoa
wa Iringa umeendelea kusimamia upimaji wa viwanja na uandaaji wa michoro ya
mipango miji ili kuwa na miji iliyopangwa vizuri.
Kauli
hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akiwasilisha
taarifa ya sekta ya ardhi mkoa wa Iringa kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Dr. Angelina Mabula ofisini kwake hivi karibuni.
Masenza
alisema “usimamizi wa miji na uandaaji wa
mipango ya matumizi bora ya ardhi umeendelea kufanyika na kusimamiwa katika Halmashauri
zote za Mkoa. Ili kuhakikisha kunakuwepo na miji iliyopangwa, mkoa umeendelea
kusimamia uandaaji wa michoro ya mipango miji na upimaji wa viwanja kwa ajili
ya matumizi mbalimbali katika Halmashaauri zote za Mkoa”
Alisema kuwa jumla ya viwanja 37,463 vimepimwa
mkoani Iringa. Aliongeza kuwa katika Halmashauri ya Manispaa viwanja 21,230,
Halmashauri ya mji wa Mafinga viwanja 11,950, Halmashauri ya wilaya ya Iringa
viwanja 1,500, Halmashauri ya wilaya ya Kilolo viwanja 2,020 na Halmashauri ya
wilaya ya Mufindi viwanja 763.
Alisema
kuwa mkoa umeendelea kusimamia na kuhakikisha makazi holela na ujenzi wa
milimani unapungua na kuisha kabisa kwa kuchukua hatua madhubuti. Hatua hizo ni
kusimamia ukamilishaji wa mpango kabambe wa mji wa Iringa (Iringa Master Plan)
ili kuhakikisha maeneo yote yanakuwa na matumizi na kurahisisha usimamizi wake.
Hatua nyingine ni kuendelea kusimamia zoezi la kurasimisha makazi ya wananchi. .
=30=
No comments:
Post a Comment